Askofu Anglikana Ameitaka Serikali Kutobadili Sera ya Elimu Mara Kwa Mara

Na Ferdinand Shayo,Kilimanjaro
Askofu  Mkuu wa kanisa la Anglikana Dayosisi  ya Mount  Kilimanjaro  Dr.Stanley  Hotay ameitaka serikali kutobadili sera ya elimu mara kwa mara ili kudhibiti kiwangocha elimu pamoja na kuondoa mikanganyiko inayojitokeza  kufuatia mabadiliko hayo.

Askofu Dk. Hotay ametoa kauli hiyo   katika  uzinduzi wa shule ya sekondari bishop alpha memorial high  school inayomilikiwa na kanisa hilo anasema  mabadiliko ya sera ya elimu yamekua yakiwachanganya  wadau wa elimu hivyo ni vyema sera hizo zikaa kwa muda  badala kubadilika katika kila awamu ya uongozi.

Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha anasema  serikali itaangalia uwezekano wa kushughulikia changamoto za kisera zilizoanishwa na wadau wa elimu .

Nasha amesema kuwa serikali inatambua mchango wa taasisi za dini katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu na afya jambo ambalo linasaidia kuwahudumia Watanzania hivyo wataendelea kushirikiana na taasisi hizo.

Akizungumza katika tukio ilo Mkuu wa Mkoa wa Singida  Dk. Rehema Nchimbi amesema  wamiliki wa shule wanalojukumu kuisaidia serikali kwa  kutoa elimu bora yenye maadili na nidhamu .