F Bado kunatajwa kuwepo kwa mwamko mdogo wa watu katika uchaguzi Misri | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Bado kunatajwa kuwepo kwa mwamko mdogo wa watu katika uchaguzi Misri

Wananchi wa Misri wanaendelea na zoezi la kupiga kura ikiwa ni siku ya tatu ya uchaguzi mkuu wa urais, uchaguzi ambao rais wa sasa Abdel Fattah al-Sisi anatarajiwa kushinda kirahisi dhidi ya mgombea mwingine ambaye hajulikani sana.

Idadi ndogo ya wapifa kura imeshuhudiwa jana tena katika vituo vingi vya kupigia kura wakati ambapo vituo vilifunguliwa maajira ya 9.00 kwa saa za Cairo.

Mamlaka nchini Misri zimekuwa zikitoa wito kwa raia kujitokeza kwa uwingi kushiriki kwenye uchaguzi huu wa siku tatu, wakitarajia pengine idadi kubwa ya watu itajitokeza licha ya kuonekana tayari kuna hitimisho la nani ataibuka mshindi.

Mgombea pekee anayeshindana na Sisi, Moussa Mostafa Moussa, yeye mwenyewe anadaiwa kuwa mfuasi mkubwa wa al-Sisi na hata kujitokeza kwake kuliibua maswali.