F Bocco atetewa na Mashabiki wa Al Masry | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Bocco atetewa na Mashabiki wa Al Masry


PAMOJA na mwamuzi kutoka Eritrea kumlamba kadi ya njano nahodha wa Simba, John Bocco akimtuhumu kumkanyaga mtoto, mashabiki wa Al Masry wamepinga hilo na kusema mwamuzi hakutumia busara.

Bocco aliteleza na kuanguka wakati akiufuata mpira uliotoka. Alipoanguka alijikuta anamkanyanga mtoto muokota mipira ambaye alilazimika kupata matibabu.

Baada ya mechi mashabiki wa Al Masry walionekana wakimpa pole Bocco kutokana na kilichotokea. Wengine waliliambia Championi Jumatatu kuwa mwamuzi hakuonyesha busara kumuadhibu Bocco ambaye wanadhani hakukosea.

Simba ilitoka suluhu katika mchezo huo na kutolewa kwa jumla ya mabao 2-2, baada ya kuruhusu mabao mawili ya ugenini katika mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam.