Siku za hivi karibuni ilisambaa picha ya Diwani wa Kata ya Ngarenaro wa CHADEMA Isaya Doita akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo jambo lililozua mijadala kwenye mitandao ya kijamii huku wengine wakisema hiyo ni dalili ya diwani huyo kuhama chama.
Sasa leo March 26, 2018 Diwani huyo Doita ameeleza kuwa hana mpango wa kuhama chama na kwamba alikutana na RC Gambo ili kupanga mambo ya maendeleo.
“Kwa Mkuu wa mkoa ku-post picha tuliyopiga pamoja inaonesha anatambua uwepo wangu na anatambua nina sauti kuliko yeye na anajisifia kupiga picha na mimi.” – Isaya Doita