DR Congo: Mapigano yasababisha shule kufungwa

Takriban shule ishirini zimechomwa moto kutokana na mapigano yanayoendelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kwa mujibu wa habari,ndani ya wiki mbili zilizopita shule za msingi na sekondari zimekuwa zikiangamizwa kwa moto katika mapigano ya kikabila kaskazini mashariki mwa DRC.

Afisa polisi Ivan Legu amekiambia kituo cha habari cha Anadolu kuwa zaidi ya shule 60 zimefungwa katika vijiji sita eneo la  Djugu,Ituri.

Hii ni kutokana na mapigano na mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanywa kati ya jamii za Lendu na Hema.

Zaidi ya watu arobaini wamepoteza maisha katika mapigano hayo,hali iliyoilazimu serikali kutuma majeshi kutuliza ghasia lakini bado haikusaidia.

Eneo la Ituri linaongoz katika mapigano ya kikabila na kusababisha vifo vya wengi.