Manchester United imepangwa kucheza na Tottenham Hotspurs kwenye hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA.
United ilishinda mchezo wake wa mwisho baada ya kuiondoa Brighton FC, wakati Tottenham yenyewe ilipata matokeo dhidi ya Swansea City, Jumamosi ya wiki hii.
Mbali na United kukutana na Tottenham, Chelsea nayo imepangwa kukipiga dhidi ya Southampton iliyoitoa Wigan Athletic kwenye mashindano hayo.
Chelsea imefika hatua hii baada ya kutoshana nguvu mpaka muda wa dakika za ziada 'Extra Time' leo dhidi ya Leicester City na kupata matokeo ya mabao 2-1.
Timu hizi zimepangwa kukutana kufuatia droo iliochezshwa jana Machi 18 2018.