F Dullah Makabila amuweka katika hali tete Tiko | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Dullah Makabila amuweka katika hali tete Tiko

Msanii wa muziki wa Singeli, Dullah Makabila

BAADA ya habari na picha za msanii wa muziki wa Singeli, Dullah Makabila na msanii wa filamu Bongo, Tiko Hassan kuzagaa wakiwa kimahaba, habari mpya ni kwamba ishu hiyo imemsababishia mwanadada huyo tafrani ya aina yake.

Rafiki wa karibu na Tiko aliieleza Za Motomoto News kuwa, mrembo huyo, baada ya picha na habari kuvuja kwamba anatoka kimapenzi na Dullah Makabila, hali ilikuwa tete kwani mpenzi wake anayemweka mjini alimjia juu na penzi lao kuwa shakani.


Tiko Hassan

“Kiukweli Tiko ameumizwa sana na Makabila ambaye alivujisha picha kwani ana mpenzi wake ambaye ndiye anayemweka mjini hivyo baada ya kuona habari hizo kuliibuka gogoro zito na kushindwa kuelewana kabisa yaani mpaka sasa Tiko anaendelea kuomba msamaha kwa bwana’ke maana huyo Dullah anasema ni rafiki yake wa kawaida tu,” alisema mtoa habari huyo.

Alipoulizwa Tiko kuhusiana na hilo alisema ni kweli picha na habari hizo zilizua tafrani kubwa kwa mpenzi wake akitaka kujua imekuwaje na mpaka sasa bado mambo hayajakaa sawa.

“Yaani mpenzi wangu alikasirika sana kwa kweli maana aliona picha na habari kwenye mitandao na gazetini, gogoro lilikuwa kubwa na mpaka sasa ninaendelea kumwelewesha kwamba Dullah siyo mtu wangu, bali ni rafiki yangu wa kawaida na zile picha tulipiga tu kama utani, lakini siyo mpenzi wangu,” alisema Tiko.