F Faida za kujua unachokitaka (lengo lako) katika maisha | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Faida za kujua unachokitaka (lengo lako) katika maisha

Kimsingi kila  mwanadamu anapenda kuwa na maisha mazuri siku zote,  hakuna hata mmoja ambaye anapenda kuiishi katika maisha ambayo  sio mazuri hata siku moja. Baadhi wa watu hasa ambao hawajafanikiwa  ukiwauliza kile ambacho wanakihitaji, wengi wao hutoa majibu ya ujumla kwamba nataka kuwa mfanyabiashara, nataka kusoma , nataka kujenga nyumba na vitu vingine vingi ambavyo mwanadamu huyu anataka kuwa  au kuvifanya kwa hapo baadae.

Lakini ukweli ni kwamba kusema hayo huwa tunakosea kwa sababu huwa tunayoongelea kwa mapana sana, hapa namaanisha ya kwamba lengo lako la kesho lazima liwe maalaumu na liwe limeandaliwa na siku yako ya leo. Kwa mfano usiseme unataka kuwa mbanyabishara na kuishia hapo tu, bali ni lazima uainishe ni aina gani ya biahara unayotaka kuja kuifanya na utie nia ya kweli juu ya biashara hiyo. Kwa mfano unaweza kupanga malengo yako ya hapo baadae unataka kuwa mfanyabiashara wa viatu, nguo za kiume,kike ,viatu vya watoo n,k.  vilevile Hata kama unataka kujenga nyumba katika mipango y yako lazima ufikirie  unataka nyumba ya aina gani? Iwe na vyumba vingapi, aina gani ya madirisha unatamani yawe kwenye nyumba yako na vitu vingine vingi ambavyo vinatakiwa katika hiyo nyumba.

Hebu tuone faida ya kujua kile unachokitaka katika masiha yako

Huongeza kujiamini.
Baada ya kujua ni nini ambacho unakihitaji katika maisha yako. Itakusaidia sana kuweza kujiamini kwa kuweka jitihada za dhati za kufikiri na za kiutendaji katika jambo hilo. Mfano wewe ni mwanafunzi umejua ni nini ambacho unakihitaji katika masomo yako. Ni matumaini yangu makubwa utajenga uwezo mkubwa wa kujiamini na kufanya vizuri katika masomo yako ili aweze kutimiza ndoto zako, halikadhalika wewe unayetaka kuwa mfanyabiashara  na watu wengineo ni lazima ujiamini katika jambo lako kwani Kujiamini ni siri kubwa kwa mtu yeyote msaka maendeleo kuweza kufanikiwa. Baada  kujua ni nini ambacho unakitaka kutakusaidia sana   kuweka mikakati na mipango ili kutimiza lengo mahususi.

Humfanya mtu kutokupoteza nguvu nyingi katika masuala ambayo hayana faida kwake.
Mtu akijua anachokitaka mara nyingi huwa ni mtu ambaye anajali sana muda katika kutekeleza mambo yake. Vitu  ambavyo kwake havina faida  huachana navyo mara moja.  Kama mpaka dakika hii unatumia nguvu nyingi kwa kitu ambacho hakina manufaa kwako jaribu kukiacha kitu hicho na anza kufanya vitu ambavyo vitakuwa na manufaa makubwa kwako. Kwenye vitu ambavyo ni kweli unavitaka jaribu kuwa makini katika matumizi sahihi ya muda ili kuweza kupata matokeo mazuri  juu ya jambo hilo.

Mara kwa mara mtu ambaye anafanya vitu ambavyo anavipenda huangalia zaidi katika masuala yatakayomletea faida tu. Ila mawazo na mitazomo ambayo haina faida huachana nayo.
Huleta hamasa kubwa ya kiutendaji.

Ukifanya kitu unachokipenda mara nyingi huleta matokeo makubwa sana. 
Mfano wanafunzi wengi hawafanyi vizuri kimasomo kwa sababu wanasoma vitu ambavyo siyo chaguo lako. Mtu anapenda kusoma masomo ya biashara lakini wanampangia akasome sayansi, matokeo yake mtu huyu akifeli tunaanza kumlaumu kwamba  hana akili kumbe tatizo ni kumchagulia vitu asivyovitaka.

Halikadhalika hata kwa wafanyabiashara walio wengi, 
biashara zao zinakufa hii ni kutokana wanafanya biashara ambazo sio chaguo lao sahihi mwisho wa siku biashara hizo huzidumu. Moja ya kutaka kuona mafanikio ya kibiashara, elimu na vitu vingine hakikisha ya kwamba unafanya vile ambavyo kweli unavipenda kutoka moyoni mwako.

Kwa kuwa mafanikio yako yapo mikononi mwako, fikiri kwa makini mambo ambayo unahisi ni chaguo lako sahihi, na ukiyafanya kwa umakini wa hali ya juu utafanikiwa. Daima kumbuka usemi huu wa ushindi siku zote my wish is my command.

Asante sana kwa kuendelea kufuatila makala kutoka katika mtandao huu , ombi langu kwako washirikishe wenzako kadri uwezavyo ili wajifunze zaidi.