Mrembo Wema Sepetu ametoa sababu ni kwanini kila mara anapenda kuposti picha za watoto tofauti tofauti katika ukurasa wake wa Instagram.
Ameeleza hayo baada ya kufanya mugizaji Idris Sultan kumwambia; si uanzishe tu nursery, Mrembo huyo aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2006 hakukawia kujibu comment hiyo ya Idriss, ni kama alichokozwa alivyoijibu kwa haraka;
Dah… mbona ningekuwa nae wa kwangu ningekuwa nampost all the time… ni kwasababu tu sina wangu… so i post every baby dat melts my heart…
Since i don’t have one to call my owm… ila ningekuwa nae mbona ungeni-unfollow… Smh…
Utakumbuka mwaka 2016 Idris na Wema walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na ilifikia hatua wakaeleza kuwa wanatarajia kupata watoto mapacha, hata hivyo baadae ilikuja kuripotiwa kuwa ujauzito huo kuharibika.