F Kilimo Bora Cha Maharage | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Kilimo Bora Cha Maharage

Related image

Maharage ni zao jamii ya mikunde ambalo hulimwa kwa ajili ya kuliwa kama mboga au futari. Mlo huu unaweza kupukwa pale ambapo maharage mabichi au maharage makavu. Pia majani yake huliwa kama chakula cha mifugo na binadamu pia. Maharage hulimwa kwa kwa wingi Mbeya, kigoma, arusha, moshi, morogoro na mikoa mingineyo.

HALI YA HEWA
Hustawi vizuri maeneo yenye mwinuko wa mita 1000 hadi 2000 kutoka katika usawa wa bahari . Pia yanaweza kulimwa pungufu ya mita 1000 au zaidi ya mita 2000 kutoka usawa wa bahari.

Maharage huhitaji mvua ya kutosha katika kipindi cha upandaji na ukuaji pia. Maharage pia Huitaji unyevu kidogo kipindi cha kuweka maua na ukavu kipindi cha kukomaa na kukauka vitumba.


AINA ZA MBEGU BORA ZA MAHARAGE
Kuna aina mbalimbali za mbegu bora za maharage kama vile canadian wonder, uyole, SUA, ilonga na lyamungo.


UPANDAJI
Maharage hupandwa mwishoni mwa msimu wa mvua kuepusha kunyeshewa kipindi cha uekaji maua.Yanawezwa kupandwa mwezi Februari,machi,aprili inategemea mvua katika eneo lako zinaisha mwezi gani.

Fukia mbegu zako katika shimo kwa vipimo vya  sm2.5 hadi 4 katika ardhi kutegemea na aina ya udongo shambani kwako.


NAFASI YA UPANDAJI
Maharage yapandwe kwa nafasi ya sentimeta 40-60 mstari hadi mstari na sentimeta 8 -15 shina hadi shina.


MBOLEA
Unaweza kupanda katika shamba lililotawanywa mbolea ya samadi.
Pia uanweza kwa uzuri zaidi kupandia mbolea za viwandani kama vile TSP  kwa kiasi cha kg 50 -100 kwa ekari.

Wakati wa mmea kuanza kuweka maua unaweza kutumia mbolea ya N.P.K au SA au Kwa Kiasi Kidogo CAN au UREA Angalizo Mbolea hizi zikizidi maharage huwa na majani mengi kuliko maua na kusababisha mavuno kuwa machache.

UPALILIAJI
Upaliliaji inabidi ufanyike mapema mara tuu maharage yanapoota na mara baada ya shamba  kuwa na magugu. Palizi ya kwanza inaweza kufanyika Kati ya siku 8-12 baada ya mmea kuota na palizi  ya pili ifanyike siku ya 20- 30 baada ya palizi ya kwanza. Kufanya hivi husaidia kuyarinda maua ya maharage yako yasipukutike wakati wa palizi hakikisha unaepuka palizi kipindi cha uwekaji maua.



WADUDU
Funza wa maharage ni wadudu wanaoshambulia mimea michanga ya maharage. Funza wa maharage hawa huweza kusababisha uharibifu hadi kufikia asilimia 100 kufuatana na hali ya hewa-unyevu kidogo, rutuba kidogo, kuwepo kwa maotea ya aina ya maharage na magonjwa kwenye udongo, kurudia kupanda zao la maharage kila msimu na aina ya maharage.

Njia nzuri ya kudhibiti funza wa maharage ni:-

  1. Kupanda mapema
  2. Kupakaza mbegu dawa kama endosufan, Acephate, Murtano kabla ya kuoanda mbegu ardhini. Kufanya hivi kutasaidia  kuzuia funza wa maharage na visababishi vya kuozesha mizizi.


Pia maharage yanaweza kushambuliwa na wadudu mbalimbali kama vile nzi weupe wa maharage na wengineo ambao wanweza kuzuiwa kwa kutumia dawa mbalimbali za wadudu.


MAGONJWA
Magonjwa maarufu ni adui katika ukuaji maharage, madoa pembe, kutu, magonjwa yanayosababishwa na bacteria na virusi. Mbegu iliyoambukizwa, udongo na takataka za maharage ni vyanzo vikubwa vya uambukizaji kwa magonjwa yote isipokuwa ugonjwa wa kutu ya majani.

UVUNAJI
Maharage huvunwa mara tuu yanaponza kukauka na kabla vitumba havijapasuka.Ng'oa mashina ya maharage na na usupige kuyaondoa katika vitumba vyake.

katika ekari moja unaweza kupata Kg 600 hadi 1200 za maharage

KUHIFADHI
Baada ya kuyapiga na kupeta kuondoa uchafu yaanike juani kwa siku kazaa kuhakikisha yamekauka na hayana unyevu unaoweza kusababisha yapate fangasi. Yahifadhi katika magunia,kama yatakaa muda mrefu bila kuliwa basi hakikisha unayahifadhi kwa kutumia dawa za kuulia wadudu kama vile Shumba, Kama vile ACTELLIC DUST au MALATHION. au Tumia mifuko maalum ya kuhifadhia nafaka. Mifuko hii huwa na maalumu ambayo husaidia kuzuia wadudu waalibifu.