Kuelekea mchezo wa robo fainali wa Kombe la Shirikisho nchini dhidi ya Njombe Mji, kocha mkuu wa Stand United, Mrundi Niyongabo Almasi ametoa angalizo kwa wapinzani wao hao kwani wamefanya maandalizi kwaajili ya ushindi tu.
“Tumejiandaa kuhakikisha tunafanya vyema katika mchezo ili tushinde tuingie katika nusu fainali na lengo letu ni kucheza fainali kisha tupate nafasi ya kuwakilkisha nchini mwakani hivyo Njombe Mji waje wakijua tumejipanga'', amesema.
Aidha Niyongabo ameongeza kuwa hata timu nyingine kwenye michuano hiyo zijipange kwakuwa timu hiyo imejipanga kuhakikisha inafanya maajabu ya kuchukua ubingwa wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza.
Stand watakuwa wenyeji wa Njombe Mji FC Machi 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, mjini Shinyanga kwenye mchezo huo ambao utaamua nani anakwenda nusu fainali ya (ASFC).