F Lema afunguka kuhusu mkakati juu ya kina Mbowe | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Lema afunguka kuhusu mkakati juu ya kina Mbowe

Mbunge wa Arusha Mjini, Mh. Godbless Lema amefunguka kwamba anafahamu kuwa upo mkakati wa kuwafunga Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine waliowekwa mahabusu tangu jana.

Katika mkutano wa Kamati Kuu ya CHADEMA uliofanyika leo na wanahabari, Lema amesema kwamba kwa haya yanayoendelea kuhusu viongozi wa Chadema.

Lema amesisitiza hana uhakika kama Mh. Mbowe na mwenzake wanaweza kupata dhamaa kwa siku ya kesho kwa sababu mkakati unaopangwa kwa ajili yao hautoki katika ofisi ndogo.

Aidha Mbunge huyo amesema kwamba Mkakati wanaoufahamu mpaka sasa kutoka katika vikao  ni kuhakikisha kina Mbowe wanafungwa haraka kama ilivyofanyika kwa Mbunge Sugu.

Mbunge huyo ameweka wazi kwamba yapo mengi yanaoyoendelea katika ofisi nyingi za serikali wanayafahamu na ndiyo maana katika Waraka wa Mbowe waliandika 'asante teknolojia kwa sababu inamaana kubwa sana'.

Ameongeza kuwa watyaweka mambo yote hadharani kwani kila kinachoendelea kwa viongozi hao kilipangwa na kushinikizwa