Sunday Mangu ‘Linex’
MSANII wa Bongo Fleva, Sunday Mangu ‘Linex’, ameibuka na kufungukia tetesi zinazozagaa dhidi yake kuwa ulevi ndiyo umempoteza kimuziki na kusema siyo kweli bali wanaozungumza hivyo ni wabaya wake ambao hawana nia nzuri kwake.
Akipiga stori na Risasi Vibes, Linex alisema kuwa muziki ni kama biashara nyingine na mtu anaweza kushuka na kupanda hivyo kilichompoteza ni changamoto za maisha kuwa nyingi na kushindwa kuzimudu ila anaamini atarejea tena na kuwa kama alivyokuwa zamani.
“Wanaosema kwamba nimepotea kimuziki kisa ulevi hawana nia njema na mimi, mwanamuziki yeyote anaweza kupotea bila kujali umaarufu alionao, ndiyo maana hata Bill Gates leo anaweza kuwa namba moja kwenye listi ya matajiri duniani na baada ya muda hata kwenye kumi bora akawa hayumo tena,” alisema Linex.