Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan jana ameanza ziara ya siku tatu Pemba ikiwa na lengo la kuhamasisha shughuli za maendeleo.
Makamu wa Rais ambaye amewasili Pemba jana na kupokelewa na viongozi mbali mbali wa Serikali na Chama ambapo alipokea taarifa za mikoa miwili ya Pemba. Pia Makamu wa Rais alizuru kaburi la Dkt. Omar Ali Juma lililopo Wawi, Pemba na kuweka shada la maua.
Aidha Makamu wa Rais aliwataka Wananchi wa Chumbageni kukumbuka historia na kurudi nyumbani, Makamu wa Rais aliyasema hayo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la CCM Chumbageni Wambaa.
Leo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anatazamiwa kuendelea na ziara yake ambapo ataweka jiwe la msingi katika Kituo cha Huduma za Mama na Mtoto Shumba Vyamboni .