Baada ya mshambuliaji wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Shiza Ramadhani Kichuya kuipatia bao lapili Stars mchezo wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hapo jana siku ya Jumanne.
Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amemfananisha mchezaji, Kichuya na yule mshambuliaji hatari duniani anayekipiga Barcelona, Lionel Messi “La Pulga” kwa namna ya uchezaji wake
Kichuya alifunga bao hilo dhidi ya DR Congo dakika ya 87 akipokea pasi nzuri ya Mbwana Samatta aliyefunga bao la kwanza na la 15 kwenyemichezo 40 aliyoitumikia Taifa Stars.