Ligi Kuu Spain inaendelea tena leo kwa mechi kadhaa kupigwa kwenye viwanja tofauti nchini humo. Moja ya michezo inayosubiriwa kwa hamu ni ule wa Sevilla dhidi ya FC. Barcelona ambao watakuwa wageni kwenye Uwanja wa Ramón Sánchez Pizjuán Stadium.
Sevilla wanakumbukwa kwa kuiota Manchester United katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mbingwa Ulaya kwa jumla ya mabao 2-1. Kibarua hicho cha leo dhidi ya Barcelona kitaanza usiku wa leo kwenye majira ya saa 3 na dakika 45. Mbali na mchezo, mechi nyingine inayosubiriwa na wapenzi wa soka nchini Spain na pande tofauti duniani ni Las Palmas itakayokuwa mwenyeji dhidi ya Real Madrid. Mechi itaanza saa 1 na nusu usiku. Mechi ambayo imekwisha malizika ni kati ya Girona dhidi ya Levante kwa sare ya bao 1-1. Mchezo unaondelea hivi sasa ikiwa ni dakika ya 15 ni Athletic Bilbao ambao wapo nyumbani wakiikaribisha Celta Vigo, matokeo bado ni 0-0.