F Mganda awagaragaza Diamond na Davido kwenye tuzo za Nickelodeon | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mganda awagaragaza Diamond na Davido kwenye tuzo za Nickelodeon


Jana usiku nchini Marekani kulikuwa na ugawaji wa tuzo za kimataifa za Nickelodeon ambapo mastaa nguli kutoka Afrika walikuwa wanachuana kuwania tuzo hizo.

Mastaa hao ni Diamond Platnumz, Cassper Nyovest, Davido, Emannuella na Eddy Kenzo ambao wote walikuwa wanachuana kwenye kipengele cha Favourite African Star 2018 ambapo Eddy Kenzo ameibuka kidedea kwa kunyanyua tuzo hiyo.

Tuzo hiyo ambayo watu wengi walibashiri kuwa mtoto mwenye kipaji cha kipee barani Afrika, Emmanuella angeibuka kidedea, imezua gumzo nchini Nigeria kwa watu wengi kuhoji ushindi wa Eddy Kenzo.