F Mimi Mars: Sitaki kuolewa na Mpare | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mimi Mars: Sitaki kuolewa na Mpare


Msanii ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake kipya 'Sitamani' chini ya Mdee Music, Mimi Mars amesema hawezi kujihusisha mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwenye kabila la Mpare kwa madai makabila hayo wanatabia ya ubahili na kujisikia.

Mimi amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuulizwa swali na ripota wa kipindi hicho kuwa anatamani mwanaume wa kabila gani ambaye awe naye katika mahusiano au ndoa.

"Kutokana na mimi mwenye kuwa ni Mpare kwa hiyo tabia za wanaume wa kipare ninazifahamu vizuri halafu wanasema mafahari wawili hawezi kukaa zizi moja hivyo najua tutashindwana tu kwasababu wote tunajisikia, wabahili 'so' tukikaa wawili 'type' hiyo mambo yatakuwa magumu", amesema Mimi Mars.

Pamoja na hayo, Mimi ameendelea kwa kusema "inanibidi nitafute kabila ambalo tofauti na mimi ndio maana sitoweza kuwa kabila hilo ila sio kwa ubaya ila mimi mwenyewe tu nimesema sitoweza.