F Mlo Kamili kwa Wagonjwa Waishio na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mlo Kamili kwa Wagonjwa Waishio na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi

Tunapozungumzia Mlo kamili huwa tunamaanisha  huwa na chakula mchanganyiko na cha kutosha na unatakiwa kuwa na chakula angalau kimoja kutoka katika makundi yafuatayo ya vyakula:-

1. Nafaka, mizizi na ndizi
Vyakula hivi huchukua sehemu kubwa ya mlo na kwa kawaida ndio vyakula vikuu. Kundi hili hushirikisha mahindi, ulezi, mchele, ngano, mtama, uwele, viazi vikuu, viazi vitamu, viazi mviringo, mihogo, magimbi, ndizi n.k.

2. Vyakula vya mikunde na vyenye asili ya wanyama
Vyakula vilivyoko kwe n ye kundi hili ni pamoja na kunde, njegere, maharagwe, njugu mawe, fiwi, soya, karanga, dengu, choroko, aina zote za nyama, mayai, maziwa, dagaa, samaki, jibini, na wadudu wanaoliwa kama kumbikumbi na senene.

3. Mboga-mboga
Kundi hili lina aina zote za mboga za majani kama matembele, mchicha, majani ya maboga, majani ya kunde, kisamvu, figiri, spinachi, sukuma wiki, mnafu, mchunga pia mboga nyingine kama karoti , biringanya, bamia, maboga, matango, pilipili hoho, nyanya chungu, mlenda, bitiruti n.k.