MDADA anayefanya kazi ya kuigiza kwenye filamu za Kibongo, Ester Kiama amesema kuwa sasa hivi yuko kwenye mfungo wa Kwaresima kwa ajili ya maombi maalum ya kutafuta mtoto wa kike.
Akizungumza na Risasi Jumamosi, Ester aliweka wazi kuwa, anatamani sana mtoto na kwa sababu tayari ana mtoto wa kiume, anahitaji kupata wa kike na ndio maana yuko kwenye mfungo maalumu wa siku 40 kwa ajili ya maombi hayo.
“Katika kipindi hiki cha Kwaresima na mimi nimefunga na kuomba, ombi langu kwa Mwenyezi Mungu ni la kutaka kupata mtoto wa kike maana ndilo hitaji langu. Ndiyo maana nimejitahidi kufunga kuanzia mwanzo mpaka nimalize 40,” alisema Ester.