F Mtoto wa Weah aweka rekodi hii | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mtoto wa Weah aweka rekodi hii

MTOTO wa Rais wa wa Liberia, George Weah aitwaye Timothy 'Tim' Weah akiwa na umri wa miaka 18 jana ameichezea kwa mara kwanza timu ya taifa ya wakubwa ya Marekani katika ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Paraguay.

Tim anafuata nyayo za baba yake, Weah ambaye ni Mwanasoka Bora wa Dunia wa FIFA mwaka 1995, anayekuwa mchezaji wa kwanza aliyezaliwa miaka ya 2000 kuichezea timu ya wakubwa ya Marekani.

"Hiki ndicho nimekuwa nikikisubiri kwa maisha yangu yote. Nimeheshimu sana nafasi niliyopewa ne benchi la ufundi la makocha, na ninatumaini kwamba nitaitwa zaidi",alisema.

Kinda huyo aliingia dakika ya 86 akitokea benchi Alfajiri ya leo katika mchezo ambao bao la penalti la Bobby Wood dakika ya 45 liliipa ushindi wa kwanza Marekani katika mechi tatu chini ya kocha wa muda, Dave Sarachan.

Weah alicheza mechi ya kwanza kikosi cha timu ya taifa ya wakubwa ya Paris Saint-Germain Machi 3, kiasi cha wiki mbili baada ya sherehe za kutimiza kwake miaka 18 ya kuzaliwa.

Alicheza pamoja na kiungo, Mmarekani mwenzake, Darlington Nagbe, ambaye baba yake, Joe alikuwa Nahodha wa Liberia na mchezaji mwenzake, George Weah.

Sarachan, ambaye alichukua nafasi ya Bruce Arena baada ya Marekani kukosa tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018, aliwapongeza vijana wake kwa ushindi huo.

Kikosi cha Marekani kilikuwa; Steffen, Yedlin, Miazga, Adams, Carter-Vickers, Nagbe/Roldan dk90, Wood/Novakovich dk77, Delgado/Weah dk86, Saief/Rubin dk67, Villafana na Trapp.

Paraguay: Fernandez, Gomez, Balbuena, Valdez, Camacho/Perez dk55, Rojas/Gonzalez dk81, Santander, Alonso, Riveros/Ortiz dk66, O. Romero/Dominguez dk81 na Almiron.