F Nape Nnauye awapa somo viongozi wa siasa | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Nape Nnauye awapa somo viongozi wa siasa

Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Moses Nnauye(CCM) amesema kuwa viongozi wa kisiasa wasipojijengea utamaduni wa kuvumiliana Tanzania itakuwa nchi ya ovyo kabisa kuishi.

Nape amesema hayo kwenye mtandao wa kijamii huku akitoa salamu za pole kufuatia cha Mzee Victor Kimesera huku akieleza kuwa kwa mzee huyo wanajifunza siasa za kuvumiliana.

“Pumzika Mzee Kimesera, kwako tunajifunza siasa za kuvumiliana! Viongozi wa kisiasa tusipojenga Utamaduni wa Kuvumiliana Tanzania itakuwa nchi ya hovyo kabisa kuishi!,“ ameandika Nape katika ukurasa wake wa Twitter.

Victor Kimesera alikuwa ni mmoja wa waasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).