F Ngoma ajifua na wenzake | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Ngoma ajifua na wenzake

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Donald Ngoma anaendelea kufanya vizuri katika mazoezi na wenzake kambini Morogoro, baada ya kurejea kikosini akiwa amekaa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha.

Akielezea hali ya kambi mkoani Morogoro leo, meneja wa Yanga Hafidh Saleh, amesema kwamba Ngoma ambaye ni raia wa Zimbabwe anaendelea kufanya vizuri katika mazoezi ya kambi hiyo.

"Ngoma anaendelea vizuri, anafanya mazoezi yote yanayotolewa na benchi la ufundi akiwa na wenzake, hivyo kama walimu watajiridhisha na uwezo wake anaweza akacheza mchezo wetu ujao'', amesema.

Ngoma ambaye alisajiliwa na Yanga mwaka 2016 akitokea  FC Platinum ya Zimbabwe amekuwa nje kwa muda mrefu akiuguza goti lake hali iliyosababisha kukosa mechi za ligi kuu pamoja na mechi za kimataifa ilizocheza Yanga msimu huu.

Yanga imeweka kambi mkoani Morogoro ikijiandaa na mchezo wake wa kombe la shirikisho hatua ya robo fainali dhidi ya Singida United April 1 kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.