Timu ya taifa ya Tanzania iliyo na umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) imelazimishwa sare tasa ya bila kufungana dhidi ya DR Congo kwenye mchezo wa kwanza wa kufuzu kutafuta tiketi ya kushiriki mashindano ya AFCON (U20).
Vijana wa Ngorongoro Heroes sasa watalazimika kutoka na ushindi walau wa bao 1 – 0 dhidi ya DR Congo ambao watakuwa nchini kwao Congo kwenye mchezo wa marudiano wiki chache zijazo.