F Nisha na Brown mapenzi wazi wazi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Nisha na Brown mapenzi wazi wazi


Couple mpya kwa sasa mjini ambayo imeanza kuchukua headlines zake ni Muigizaji Nisha na Brown ambaye hapo awali alikuwa akitoka kimapenzi na Jacqueline Wolper.

Wawili hao wamezidi kuachia video mtandaoni wakiwa pamoja na safari hii wanaonekana wakipeana mabusu mazito wazi wazi.

Katika video hiyo aliyoweka Nisha Instagram ameandika; kitu pekee tunachohitaji ni furaha ila mara nyingi tunaangukia kwenye vilio vya kujitakia. Washauri wa mapenzi ni wengi ila unahisi unaweza kunishauri wa kuwa naye wakati tayari moyo wangu upo sehemu fulani.

Hata hivyo kuna taarifa ambazo zinadai wawili hao kuna project wanayofanya pamoja inayokwenda kwa jina la Bachela ingawa hakuna yeyote kati yao aliyethibitisha hilo hadi sasa.