F Norah: Wapo wengi ninaowakubali Gabo namzimia kweli | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Norah: Wapo wengi ninaowakubali Gabo namzimia kweli


Nuru Nasoro ‘Norah’.

MKONGWE wa sinema za Kibongo, Nuru Nasoro ‘Norah’ amesema kati ya waigizaji wa kiume anaowakubali kutoka Bongo Movies ni muigizaji Gabo Zigamba.

Norah alifunguka hilo hivi karibuni alipokuwa akipiga stori mbili tatu na mwanahabari wetu ambapo alipoulizwa kuhusu listi ya wasanii wa kiume anaowakubali Bongo, moja kwa moja alianza kwa kumtaja Gabo.

Gabo Zigamba.

“Wapo wengi ninaowakubali na listi yangu inaongozwa na Gabo namzimia kweli. Wengine ninaowakubali ni JB, Frank Mwikongi, Chiki Mchoma na Dude,” alisema Norah.

Alipoulizwa nini kinamvutia zaidi kwa waigizaji hao, alisema ni namna wanavyojua kubadilika kulingana na matakwa ya filamu husika.