Polisi Njombe yajipanga na sikukuu za Pasaka

Jeshi la polisi mkoani Njombe limesema litafanya doria za aina tatu katika miji yote ya mkoa wa huo hasa katika maeneo tata ambayo wana wasiwasi wa kutokea kwa vurugu wakati wa sikukuu za Pasaka na kushirikiana na vyombo vingine vya usalama.

Hayo yamebainishwa na Kamishina Msaidizi wa Polisi, SACP Renata Mzinga wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari na kusema jeshi hilo litafanya doria kwa kutumia magari, pikipiki pamoja na miguu katika kulinda hali ya usalama katika kipindi hiki cha Sikukuu.

"Niwape tahadhari wakazi wa mkoa wa Njombe, waepuke kujazana katika kumbi za starehe ili kujiepusha na vifo vinavyotokana na kukosa hewa kama ilivyotokea miaka ya nyuma mahara pengine hapa nchini", amesema SACP Mzinga.

Kwa upande mwingine, Kamanda Mzinga amewataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwa kuwa kitendo hicho ni uvunjifu wa sheria.