Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amefunguka na kudai hata adharauliwe kwa kiasi gani hawezi kuthubutu kutamani au kujilinganisha maisha yake na mtu mwingine kwa kuwa anaimani kila mmoja Mungu amempangia fungu lake.
Shamsa ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa kijamii ikiwa kama somo au fundisho kwa baadhi ya watu wenye tabia ya kupenda kutamani na kujilinganisha maisha na watu fulani waliowazidi uwezo na matokeo yake huwa wanaishia kuaibika kutokana na wanachokifanya hakipo katika uwezo wao.
"Huwa naishi maisha ninayoyaweza siku zote, sitamani vya watu wala kulinganisha maisha yangu na mtu yeyote kwasababu huwa naamini Mwenyezi Mungu amempa kila mtu kwa wakati wake na kila mtu ana kalma yake", amesema Shamsa.
Pamoja na hayo, Shamsa Ford ameendelea kwa kusema "hata unidharau mpaka kunitemea mate kwa kuhisi una vikubwa kuliko nilivyo navyo mimi, huwa siumii kwasababu naamini Mungu amenipa maisha mazuri ingawa kwako unaona ni mabovu".
Kwa upande mwingine, Shamsa Ford amewashauri walimwengu 'jamii' wawe na tabia ya kujipenda na kujitathimini wao wenyewe binafsi hata kama ikitokea mtu akamdharau kiasi gani.