F Sierra Leone: Mahakama ya juu yaondoa amri ya kuzuia duru ya pili ya uchaguzi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Sierra Leone: Mahakama ya juu yaondoa amri ya kuzuia duru ya pili ya uchaguzi

Mahakama ya juu nchini Sierra Leone imeondoa amri inayochelewesha kufanyika duru ya pili ya uchaguzi nchini humo ikiwa ni siku mbili baada ya kusimamisha uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Jumanne.

Wanasheria wa tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo wamesema amri ya kuzuia duru ya pili ya uchaguzi tayari imesababisha mkwamo nchini humo.

Duru ya pili ya uchaguzi itashuhudia mgombea wa chama tawala Samura Kamara akichuana na mgombea wa upinzani Julius Maada Bio.

Mgombea huyo wa Upinzani alishinda kwa asilimia 43.4 ya kura kufuatia uchaguzi uliofanyika awali dhidi ya mshindani wake Samura Kamara aliyepata asilimia 42.7

Kutokana na kwamba hakukua na mgombea aliyepata asilimia 55 ya kura zilizokuwa zinahitajika kutangazwa mshindi uchaguzi huo ulilazimika kwenda katika dulu ya pili iliyopangwa kufanyika Machi 27.