Shirikisho la soka nchini TFF kupitia Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), leo limetangaza ratiba ya michezo ya ligi kuu iliyobaki ikiwemo pambano la marudiano la watani wa jadi Simba na Yanga.
Ratiba hiyo imetangazwa na Mtendaji Mkuu wa bodi hiyo Bw. Boniface Wambura ambapo amesema mchezo huo wa Simba na Yanga utachezwa April 29.04.208 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo Simba ndio itakuwa timu mwenyeji baada ya ule wa raundi ya kwanza uliochezwa Oktoba 28 2017 ambapo Yanga ilikuwa mwenyeji kumalizika kwa sare ya 1-1. Bao la Simba lilifungwa na Shiza Kichuya wakati Obrey Chirwa alifunga bao la Yanga.
Pamoja na mchezo huo wa watani wa jadi bodi pia imetangaza michezo ya viporo ya Simba na Yanga ambapo Simba itaanza kucheza na Njombe Mji April 3 kisha Mtibwa Sugar April 9.
Wakati Yanga wenyewe wataanza kucheza mechi zao za viporo baada ya mchezo wa mtoano wa kuwania kutinga hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika ambapo watacheza na Welayta Dicha ya Ethiopia Aprili 7 Uwanja wa Taifa.