Mlinzi wa timu ya taifa ya Brazil, Thiago Silva, amesema Brazil inahitaji heshima zaidi duniani na sio kubezwa kwasababu ilipoteza kwa mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani kwenye fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.
Thiago ambaye ni nahodha wa PSG ya Ufaransa ameyasema hayo baada ya kikosi chao kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ujerumani kwenye mchezo wa kirafiki wa Kalenda ya FIFA uliopigwa mjini Berlin.
"Tunaiheshimu sana Ujerumani lakini hii jezi ya Brazil inastahili heshima zaidi, tunafurahi kuwa tumeanza kuirudisha heshima ambayo dunia nzima ilikuwa imeanza kuipoteza na kuidharau timu hii yenye kila historia katika mchezo wa soka'', amesema.
Naye mashambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus ambaye ndiye mfungaji wa bao la jana usiku amesema, "Ninafurahi sio tu kwa sababu nimefunga bao, lakini pia kwa namna ambavyo hamu yangu ya kusaidia timu imetimia na nitaendelea kufanya hivyo''.
Katika mchezo wa jana Brazil ilikuwa bila ya nyota wake Neymar Jr sawa na mwaka 2014 wakati inapoteza 7-1 nyumbani ambapo pia mshambuliaji huyo wa PSG alikuwa majeruhi kama ilivyo sasa.