F Timbulo afunguka kutohofia kufungiwa Muzuki | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Timbulo afunguka kutohofia kufungiwa Muzuki

Ally Timbulo

LICHA ya baadhi ya wanamuziki kufungiwa nyimbo zao na serikali kutokana na kuwa kinyume na maadili, msanii wa Bongo Fleva, Ally Timbulo ameeleza kwamba hana hofu na hilo kwani muziki wake ni wa Kiafrika zaidi.

Akistorisha na Risasi Vibes, Timbulo alisema muziki wake una asili ya Kiafrika na siyo asili ya Ulaya kama wanamuziki wengi wanavyofanya ambao wanaacha maungo nyeti wazi au kucheza kihasara hivyo hana hofu kabisa kwamba serikali itamfungia.

“Sina muziki wenye asili ya Ulaya, muziki wangu ni wa Kiafrika, kwa hiyo sina shaka na kufungiwa maana hata video zangu nafanya zenye maadili yanayotakiwa ambapo zinaangaliwa na wakubwa kwa wadogo,” alisema Timbulo.

Hata hivyo aliwataka wasanii wenzake kufuata utaratibu kwani kila mahali kuna utaratibu na sheria zake hivyo inawapasa kuzingatia hilo ili kuweza kusonga mbele zaidi.