Watu 12 waliokuwa na rangi katika machupa wameshambulia ubalozi wa Uturuki mjini Brussels nchini Ubelgiji. Taarifa zizlitolewa na wanadiplomasia wa Uturuki ni kwamba watu hao walioshambulia kwa rangi ubalozi wa Uturk mjini Brussels ni wafuasi wa kundi la kigaidi la PKK.
Tukio hilo lililtekelezwa na wahalifu hao Jumapili majira ya asubuhi katika kuta za ubalozi na ubalozi mdogo wa Uturuki nchini Ubelgiji.
Baada ya tukio hilo usafi umefanyika katika ubalozi huo.