F Uingereza yapongeza hatua ya mataifa ya ulaya na Marekani kuwafukuza maafisa wa urusi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Uingereza yapongeza hatua ya mataifa ya ulaya na Marekani kuwafukuza maafisa wa urusi

Uingereza imepongeza kile ilichosema hatua ya mataifa ya Ulaya na Marekani kuwafukuza kwenye nchi zao waliotajwa kuwa majasusi za Urusi zaidi ya 100, ikisema huu ni uelekeo mpya wa nchi za magharibi dhidi ya Urusi.

Kauli ya Uingereza inatolewa wakati huu Urusi yenyewe ikiahidi kulipa kisasi kutokana na uamuzi uliochukuliwa na mataifa hayo.

Nchi ya Ireland imekuwa ni taifa jingine ambalo limetangaza kuwaondoa wanadiplomasia wa Urusi, wakati huu mpaka sasa wanadiplomasia wa Urusi 117 wamefukuzwa kutoka kwenye matiafa 24 katika muda wa siku 2.

Wadadisi wa mambo wanasema hatua hii inakumbusha wakati wa vita vya baridi ambapo mataifa mengi yalikuwa yanatuhumiana kutuma majasusi kufanya upelelezi na baadae kupelekea kufukuzwa.