F Urusi yaunga mkono mkutano wa Korea Kaskazini na China | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Urusi yaunga mkono mkutano wa Korea Kaskazini na China

Urusi imeunga mkono mkutano kati ya rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na rais wa China Xi Jinping mjini Beijing na kusema kuwa mkutano huo ni hatua muhimu ya kuleta mabadiliko Peninsula.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi amesema nchi yake ina mpango wa kuendeleza ushirikiano na China kutatua matatizo Peninsula kwa njia ya kidiplomasia.

Msemaji wa rais wa Kremlin  Dmitriy Peskov amesema kuwa hakuna mkutano wowote unaotarajiwa kufanywa kati ya rais Putin na Kim Jong Un.

Hayo ameyazungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari.