F VAR yawakwamisha Waingereza | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

VAR yawakwamisha Waingereza


Ikiwa Uingereza ndio nchi iliyokuwa kinara kwenye kudai matumizi ya teknolojia kwenye mchezo wa soka na kufanikisha kuanzishwa kwa Video assistant referee (VAR) hatimaye teknolojia hiyo imewasaidia wapinzani wao.

VAR imeisaida timu ya taifa ya Italia kusawazisha bao dhidi ya England kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye dimba la Wembley jijini London usiku wa kuamkia leo ambapo England ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0.

Dakika ya 87 mwamuzi Deniz Aytekin alilazimika kusimamisha mechi na kwenda kutazama marudio ya tukio la mlinzi wa England anayechezea Burnley James Tarkowski aliyemwangusha Federico Chiesa wa italy ndani ya eneo la 18.

Baada ya kupata uhakika wa tukio kupitia picha za marudio, mwamuzi aliamuru mkwaju wa penalti ndipo mchezaji Lorenzo Insigne akapiga na kuisawazishia Italia na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Teknolojia hiyo inatarajiwa kutumika kuamua matukio mbalimbali yenye utata kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka huu nchini Urusi, kuanzia Juni 14 hadi Julai 15 2018. Jumla ya mataifa 32 yatachuana kuwnaia ubingwa huo.