F Wakazi wa Dar waendelea kufuruhia Promosheni VUTA PUMZI KILA J’GWARA NA SAFARI NDOGO | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Wakazi wa Dar waendelea kufuruhia Promosheni VUTA PUMZI KILA J’GWARA NA SAFARI NDOGO




Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager leo imeendelea na promosheni ya Vuta Pumzi na Safari Ndogo ambapo watumiaji wa bia ya safari wameendelea kujishindia  kinywaji hicho kwenye vituo vya daladala.

Akizungumza jioni hii mmoja ya washindi, Hassani Saidi amesema kuwa amefurahi kushinda promosheni hiyo inayoendelea vituo mbalimbali kwa kila Jumatano ambapo leo inaeendelea katikakituo cha Mtongani Jijini Dar es salaam ambapo inahusisha watu walio juu ya miaka 18

"Nimefurahi sana kushinda promosheni ya kinywaji hiki cha bia ya Safari ndogo hivyo sina budi kuonyesha furaha yangu, na nawaambia watanzania wenzangu ambao wanatumiaji wa bia hii kuja katika kituo hiki ili kujishindia" Alisema Said

Mtumiaji wa bia hiyo atakwenda kwenye vituo vya Daladala/Mabasi vyenye huduma hiyo ambayo Safari Lager wameendelea kituo cha Mtongani ambapo washindi walioshinda wamepata zawadi ya bia kwenye bar ambayo ilichaguliwa kwenye kituo.


Kumbuka mashine hizo zitatoa bia kwa siku ya Jumatano pekee kuanzia saa 10 jioni hadi saa 6 usiku na washindi wote watapelekwa na bajaji kwenye baa zilizo karibu na kituo husika.

Aidha Kampuni hii ya TBL kwa kuendelea kuwajali na kuthamini wateja jumatano ijayo promosheni hii itakua kwenye kituo daladala cha Tabata jijini Dar es salaam, hivyo watumiaji wafike eneo hilo ili wajishindie.