F Wananchi wagaiwa samaki bure | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Wananchi wagaiwa samaki bure

Maafisa wa Idara ya Uvuvi Wilaya ya Geita,walioko kwenye doria ya kusaka na kukamata wavuvi haramu kwenye visiwa vilivyopo ndani ya Ziwa Victoria Wilayani humo,wamefanikiwa kukamata samaki wachanga aina ya Sangara zaidi ya 2000 waliovuliwa kinyume cha Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009,kisha kuwagawa bure kwa wananchi.

Akiongea na Channel Ten mara baada ya kumaliza zoezi la kuwagawia wananchi samaki hao,Afisa Uvuvi wa Tarafa ya Bugando Wilayani Geita,Revocatus Nahonge,amesema kisheria samaki wanaotakiwa kuvuliwa ama kuliwa,kwa upande wa sangara ni sentimita kati ya hamsini mpaka themanini na tano.