Watumishi watakiwa kuiepusha serikali kupata hasara

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Joseph Kakunda amesema kwamba watumishi wa umma wanapaswa kutekeleza na kusimamia ipasavyo miradi mbalimbali, ili kuepusha serikali na hasara na athari za kiuchumi na kijamii.

Naibu Waziri Kakunda ametoa kauli hiyo na kueleza  kuwa mfanyakazi wa umma anaweza kushtakiwa kwa kosa la kiutumishi na kosa la kijinai, endapo itabainika miradi anayoisimamia imetekelezwa chini ya kiwango.

Waziri Kakunda ameendelea kusema kwamba kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki wanazotakiwa kuzipata kutokana na miradi ya maendeleo, hivyo kutosimamia kikamilifu miradi hiyo ni moja ya makosa ambayo mfanyakazi wa umma anaweza kushtakiwa.