Aliyekuwa Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady ametua nchini Tanzania kimya kimya Jumanne hii kwaajili ya kusaini dili nono na kampuni moja ya nepi za watato huku akiwazidi kete mastaa wa kike Tanzania.
Mapema asubuhi leo (March 28 2018) mrembo huyo aliutaarifu Umma wa Tanzania kwamba yupo nchini Tanzania kwaajili ya kusaini dili hilo.
Muda mchache baadaye Zari alionekana katika mitandao ya kijamii akisaini dili hilo ambalo bado halijajulika thamani yake huku wadau wa mambo wakidai huwenda dili hilo ni nono kutokana na mrembo huyo kuwa na umaarufu Afrika Mashariki.
Zari mapema mwaka 2017 alisaini mkataba mzito na kampuni ya Danube ambayo inamiliki maduka makubwa ya nguo nchini Tanzania.
Zari akiwa nchini Tanzania ameonekana kuwa na mbunifu wa mavazi Noel, huku akimtosa Diamond ambaye kwa sasa amekorofishana naye.
Mbunifu huyo wa mavazi amekuwa akitoa taarifa mbalimbali juu ya mrembo huyo hata taarifa ya dili hilo alilitoa yeye kupitia Instagram.
“Done deal she is official,” alindika Noel.