F Baada ya kutolewa kwenye michuano Yanga kurejea Dar | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Baada ya kutolewa kwenye michuano Yanga kurejea Dar


Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho jana dhidi ya Singida United, kikosi cha Yanga kinatarajia kuwasili leo Dar es Salaam.

Yanga ilishindwa kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kukubali kichapo cha matuta (4-2) kutoka kwa walima alizeti hao, hiyo ilikuwa ni mara baada ya dakika 90 kwenda sare ya 1-1.

Yanga inarejea Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Welayta Dicha FC ya Ethiopia utakaopigwa Jumamosi ya wiki hii Uwanja wa Taifa.

Endapo Yanga itafanikiwa kuingia hatua ya makundi katika michuano ya Shirikisho Afrika, itajitwalia kiasi cha milioni 600 kutokana na taratibu za CAF zilivyo ambapo kila anayeingia hatua hiyo hupewa kitita hicho cha pesa.