F " Hatuna taarifa ya Rais kushinda tuzo" Ikulu | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

" Hatuna taarifa ya Rais kushinda tuzo" Ikulu

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, nchini Bwana Gerson Msigwa, amesema haiana taarifa juu ya tuzo aliyoshinda Rais John Magufuli nchini Ghana, kama kiongozi bora barani Afrika.

Akizungumza na www.eatv.tv Msigwa amesema kuwa utaratibu wa tuzo yoyote lazima mtu anayepewa apewe taarifa rasmi, lakini mpaka sasa hawajapokea taarifa yoyote kutoka kwa waandaaji wa tuzo hizo, hivyo hawajui lolote kama ni kweli ama la.

“Hatuna taarifa ya tuzo hiyo, tunavyojua ni kwamba mtu yeyote anayepewa tuzo lazima apewe taarifa rasmi kutoka kwa watoaji, sasa hatujapata taarifa yoyote mpaka sasa, nasikia ndio tuzo ambazo kina Monalisa wameshinda, lakini hatujapokea taarifa rasmi kuhusu tuzo hiyo, hivyo siwezi nikaizungumzia”, amesema Msigwa.

Tuzo hiyo ambayo imetajwa kuwa ameshinda Rais Magufuli, imetolewa Aprili 15, 2018 jijini Accra nchini Ghana, ambapo pia Watanzania wengine katika tasnia ya filamu waliibuka washindi akiwemo Monalisa (Yvone Chery) na Ray Kigosi.

EATV.