F Idadi ya Watoto waliozaliwa leo yatolewa Muhimbili | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Idadi ya Watoto waliozaliwa leo yatolewa Muhimbili


Jumla ya watoto 7 wamezaliwa siku ya leo Aprili Mosi, 2018, ambayo ni sikukuu ya pasaka, katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

Taarifa hiyo imetolewa na ofisi ya mahusiano ya hospitali ya Muhimbili, ambapo imeeleza kwamba watoto hao waliozaliwa wanne ni kike, huku wakiume wakiwa watatu, na wazazi sita wakiwa wamejifungua kawaida na mmoja kwa upasuaji.

Mama na watoto hao wote wapo salama na wanaendelea vizuri hospitalini hapo.