F Israel yaiunga mkono Marekani | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Israel yaiunga mkono Marekani

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa nchi yake inaunga mkono mia kwa mia uamuzi wa Marekani kuishambulia serikali ya Assad.

Waziri Netanyahu amesema Israel inaunga mkono uamuzi huo wa Marekani ulioungwa mkono na Ufaransa pamoja na Uingereza.

"Tumekuwa tukiunga mkono uamuzi wa Trump dhidi ya silaha za kemikali toka mwaka mmoja uliopita",alisema Netanyahu.

Israel inaamini serikali ya Assad inapashwa kudhibitiwa vilivyo ili kuhakikisha kuwa haitumii silaha za kemikali dhidi ya halaiki.

Marekani,Uingereza na Ufaransa zimefanya shambulizi la anga dhidi ya serikali ya Assad nchini Syria.

Hii ni baada ya shambulizi baya la kemikali kutokea Douma na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 70 wengi wao wakiwa ni watoto wadogo.