F John Heche aunganishwa na Viongozi wengine wa Chadema | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

John Heche aunganishwa na Viongozi wengine wa Chadema


Hatimaye Mbunge wa Tarime Vijijini(CHADEMA), John Heche leo amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  na kuunganishwa kwenye kesi namba 112/2018 inayowakabili Viongozi wengine wa Chama  hicho.

Wakili wa serikali, Faraja Nchimbi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa wanaomba kumuunganisha Heche katika kesi inayowakabili wenzake ambapo yeye atakuwa mshtakiwa wa 8 ambapo amepewa kwa masharti ya dhamana kama watuhumiwa wengine.

John Heche  ameachiwa kwa masharti ya dhamana na anahitajika kuwasili  cha Polisi Central kila Ijumaa huku kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 16 Aprili mwaka huu.