F Lulu atoa mchango wake akiwa gerezani | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Lulu atoa mchango wake akiwa gerezani


Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye kwa sasa anaendelea kutumikia kifungo chake jela ametoa mchango wake wa Pads kwa lengo la kuwasaidia watoto wa kike katika kampeni ya Namthamini inayoendeshwa na uongozi wa EATV.

Zawadi hizo ambazo ziliwakilishwa na msanii mwenzake Mahsein a.k.a Dkt. Cheni jana (Aprili 03) katika ofisi za EATV Mikocheni Jijini Dar es Salaam na kusema anaamini kampeni hiyi itawaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye jamii ya sasa kutoka na matatizo wanayokumbana na watoto wa kike walioko mashuleni.

"Huu ni mzigo wa Elizabeth Michael (LULU), ameomba niwasilishe kwenu. Nimekuwa nikimtembelea mara kadhaa kumjulia hali na yeye ameomba ashiriki kwenye kampeni hii ingawaje hayupo. Yupo (jela) zaidi amesema niwaambie anawapenda sana, na anawataka mabinti wa kitanzania wawe huru katika kutimiza malengo yao, wasikate tamaa na Mungu atawasimamia", amesema Dkt. Cheni.

Elizabeth Michael anatumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua aliyekuwa mpenzi wake na muigizaji mwenzake Steven Kanumba bila kukusudia mnamo April 7, 2014.