F Mwigulu: Wanaoanzisha nyumba za ibada wapewe masharti mepesi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mwigulu: Wanaoanzisha nyumba za ibada wapewe masharti mepesi

Na James Timber, Mwanza
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amesema watu wanaoanzisha nyumba za ibada wapewe vibali haraka na masharti mepesi, kwani nyumba hizo zinapunguza vitendo vya ukatili na kuleta amani nchini.

Akizungumza kwenye Tamasha la Pasaka jijini hapa Kwa Niaba ya Mgeni Rasmi Makamu wa Rais  Samia Suluhu, mara baada ya uzinduzi wa albamu ya Rose Mhando iitwayo "Usivunjike Moyo" aliwataka wanaotoa vibali vya nyumba za ibaada watoe vibali haraka ili wananchi wapate huduma hiyo ya kiroho.

"Unakuta vibali vya nyumba za starehe vinatolewa ndani ya wiki moja huku vibali vya nyumba za ibada vinatoka kwa miaka kadhaa, sitapenda hali hiyo ijitokeze tena  hapa nchini, ukizingatia watu wanataka amani kupitia nyumba hizo muwapungizie masharti ya uanzishaji," alisema Waziri huyo.
Aidha aliwaomba watoa huduma katika nyumba za ibada wasihubiri kukebei, kubagua, na kutukana  imani za watu wengine kwani italeta chuki na amani haitakuepo tena.

Pia aliwashukuru waimbaji wa nyimbo za injili na kuahidi kupeleka waraka katika  mikoa yote na kuhakikisha wanaanza kuwakamata wanaofanya uhalifu wa nyimbo za injili.

Baadhi ya waimbaji waliohudumu katika tamasha hilo Boniphace Mwaitege, Martha Mwaipaja, Christina Shusho na Martha Baraka.