Kikosi cha Simba kimeanza safari asubuhi hii kuelekea Njombe tayari kwa mchezo wake wa kesho dhidi ya Njombe Mji FC.
Kikosi hicho kiliweka kambi ya muda mfupi mkoani Iringa ambapo jana kilifanya mazoezi katika Uwanja wa Samora mkoani humo.
Simba itakuwa ina kibarua cha mechi ya ligi dhidi ya Njombe Mji FC itakayopigwa kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini humo.