Tanzia: Nahodha wa England afariki

 Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya England Ray Wilkins amefariki dunia leo asubuhi kwenye hospitali ya St George's London, kwa tatizo la shinikizo la moyo. Amefariki akiwa na umri wa miaka 61.

Katika enzi zake Wilkins amewahi kuzichezea klabu za Manchester United, AC Milan, Rangers na QPR. Nyota huyo wa zamani ameacha mke wake Jackie, binti yake Jade, kijana aitwaye Ross, na wajukuu Oliver, Frankie, Ava, Freddie, Jake na Archie.

Moja ya mafanikio ambayo amewahi kuyapata ni kutwaa Kombe la FA akiwa na Manchester United mwaka 1983 na Kombe la ligi kuu ya Scottland akiwa na Rangers mwaka 1989.


Wilkins aliichezea timu ya taifa ya England mechi 84 huku akiwa nahodha katika mechi 10. Pia amewahi kuwa kocha wa timu za QPR, Fulham na timu ya taifa ya Jordan.

Nguli huyo hatosahaulika kwa kuwa kocha msaidizi wa Chelsea kutoka 1998-2000 na 2008 hadi 2010, alipokuwa akifanya kazi pamoja na Guus Hiddink na Carlo Ancelotti.