F Tiangong-1: Chombo cha anga cha China kuanguka duniani kesho Jumatatu | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Tiangong-1: Chombo cha anga cha China kuanguka duniani kesho Jumatatu


Kifusi kutoka kwa kituo cha maabara cha safari za anga cha China, kinaweza kupasuka na kuanguka duniani Ijumaa,wanasayansi wanaokifanyia uchunguzi wanasema.

Kituo hicho cha Tiangong-1 ni sehemu ya mpango wa safari za anga za mbali wa Uchina, na wa sampuli ya kituo cha safari za anga za mbali cha binadamu wa mwaka 2022.

Kiliwekwa kwenye uzio mwaka 2011 na miaka mitano baadae kikamilisha shughuli yake, na baadae kilitarajiwa kuanguka duniani.

Muda na mahala kitakapoangukia ni vigumu kutabiri kwasababu sasa hakidhibitiwi, Makadirio ya hivi karibuni ya kurejea kwa chombo hicho ni tarehe 2 Aprili.

Sehemu kubwa ya kituo hicho kina uwezekano mkubwa wa kuungua hewani, lakini kifusi kinaweza kunusurika na hivyo kuanguka kwenye uso wa dunia.

Mwaka 2016 China ilipoteza mawasiliano na chombo cha Tiangong-1 na haikuweza tena kudhibiti mienendo yake , kwa hiyo haijulikani kabisa kitaishia wapi, limesema shirika la Ulaya la safari za anga za mbali European Space Agency(ESA).

Kituo cha Esa kilitoa taarifa za mara kwa mara juu ya kituo cha Tiangong-1 na sasa kinakadiria kuwa kitaingia tena duniani baina ya tarehe 30 Machi na 2 Aprili, lakini kinasema kuwa makadiria ya muda halisi wa kurejea kwake "unatofautiana sana ".

Shirika hilo linatarajia vipimo vyake vya kurejea kwa chombo hicho vitakuwa sahihi zaidi na kulenga makadirio yake ambayo karibu na mwisho wa juma.

Kitaanguka vipi?
Kituo chenyewe kinaelekea kuikaribia dunia.

Kiwango cha kasi yake ya kushuka "kitaendelea kuwa cha haraka sana wakati hali ya hewa kwenye anga ambapo kituo hicho kimeshikia ikiendelea kuachana na kusababisha upenyo mkubwa wa chombo kuanguka," Dkt. Elias Aboutanios, Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha Australia cha Utafiti wa Safari za Anga za mbali, aliieleza BBC.

"Hatimae kituo kitaanza kuchemka kitakapoanza kukaribia umbali wa kilomita 100 kutoka duniani," anasema Dkt. Elias Aboutanios.

Hii itasababisha kuungua kwa sehemu kubwa ya kituo naanasema "ni vigumu kufahamu haswa ni nini kitanusurika kwa sababu aina ya chombo hicho haijafichuliwa na Uchina''.

Bwana Aboutanios amesema kama kitaungua wakati wa usiku katika eneo lenye wakazi wengi "kitaweza kuonekana, kama nyota ama kimondo".

Je una sababu ya kuwa na hofu?
Hapana, kwani vingi kati ya vituo vyenye ukubwa wa tani 8.5 - humeguka vinapokua hewani.

Baadhi ya sehemu nzito za chombo kama vile tenki za mafuta ama injini za roketi huenda zisiungue kabisa. Hata hivyo kama sehemu hizo zitanusurika na kuufikia uso wa dunia, uwezekano wake wa kumgonga mtu huwa ni mdogo sana.

"Uzoefu wetu ni kwamba kwa vyombo kama hivi vikubwa huwa ni asilimia 20 ama asilimia 40 yake, ndio hunusurika na kuweza hurudi duniani na kuweza kupatikana ardhini kinadharia," afisa kutoka ofisi ya vifusi vya vyombo vya anga katika shirika la safari za anga za mbali la Ulaya Esa , Holger Krag, amewaambia waandishi wa habari.

"Lakini, kujeruhiwa na moja ya vipande vyake ni jambo ambalo kwa kiwango kikubwa haliwezekani. Makadirio yangu ni kwamba kuangukiwa na chombo hiki ni sawa na uwezekano wa kupigwa na radi mara mbili kwa mwaka."

Lakini je vifusi vya vyombo vyote vya anga za mbali huanguka duniani?

Wakati vifusi vya vyombo vya anga za mabali huanguka mara kwa mara, vingi " huungua na kuishia katikati ya bahari na mbali na wanapoishi watu," anasema Bw Aboutanios.

Kwa kawaida huwa yanakuwepo bado mawasiliani na chombo au setilaiti. Hii inamaanisha kuwa udhibiti wa wataalam kutoka ardhini bado unaweza kukiongoza chombo na kukipeleka mahala ambapo wanataka kiangukie.

Kifusi huwa kinaongozwa kuangukia kwenye kile kinachoitwa ncha ya bahari ambayo haifikiwi na watu - mbali kabisa na ardhi kavu. Ni eneo lililopo Kusini mwa Pacific, baina ya Australia, New Zealand na Amerika Kusini.

Ni eneo lenye ukubwa wa kilomita za duara, 500 eneo hili ni eneo la makaburi ya vyombo vya anga za mbali pamoja na setilaiti, ambako masalia ya vyombo vya anga za mbali vipatavyo 260 yanadhaniwa kuzikwa kwenye sakafu ya bahari.

Je Tiangong-ni nini?
Uchina ilichelewa kuanza uvumbuzi wa wa anga za mbali.

Mnamo 2001, Uchina ilizindua vyombo vyake vya anga kwa kujaribu kuwatuma wanyama mwaka 2003 kwenye chombo cha anga za mbali kwenye mzingo wa dunia, na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa ni ya tatu kufanya hivyobaada ya Muungano wa Usovieti na Marekani.

Mpango wa vituo vya safari za anga za mbali ulianza kwa kukituma chombo cha Tiangong-1 ama "Kasri la Mbinguni", mwaka 2011.

Kituo hicho kidogo kiliweza kuwahifadhi wataalam wa masuala ya anga za mbali lakini kwa muda mfupi wa siku kadhaa. Mchina wa kwanza mwanamke mtaalamu wa anga za juu Liu Yang alitembelea kituo hicho mwaka 2012.

Kilikamilisha huduma zake mwezi Machi 2016, miaka miwili zaidi ya muda kiliopangiwa.